Saturday, April 20, 2013

Love Comes For Those Who have Courage


 It heart to love someone and not be loved in return, but what is more painful is to love someone and never   find the courage to let that person know how you feel. May be God wants us to meet a few wrong people before meeting the right one so that when we finally when we meet the right person we will know how to be   grateful for that gift.  Love is when you take away the feeling, the passion and the remains in the relationship and find out you still care for that person. A sad thing in life is when you meet a someone who means a lot to you and a little find out in the end that it was never meant to be and you just have to let it go.   When the door of happiness closes another opens but often times looks so long at the closed door but we don’t see the one which has been open for us. The best kind of friend is the kind you can just be with, never say a word and then work away feelings like it was the best conversation you have ever had. It is true that we don’t know what we have got until we lost it, but it is true that we also true that we don’t know what we have been missing until it arrives. Giving someone all your love is never an assurance that they we love you back.  Don’t expect love in return , just wait until it grows in their heart but if it doesn’t  be contempt it grew in yours . There are things you love to hear but you will never hear from a person whom you will like to hear them from. But don’t be so deaf as not to hear it from the one who said it from their heart. Never say goodbye if you still wants to try, never give up if you feel you can still go on, and never say you don’t love a person anymore if you can’t let it go. Love comes to those who still hope although they have been disappointed, to those who still believe although they have been betrayed, to those who still need to love although they have been hurt before and to those have courage and faith to built trust again. It takes only a minute to get crash on someone but an hour to like some and a day to love someone but it takes a life time to forget someone,. Don’t go for look  because it can deceives. Don’t go for wealth even that fades away. GO FOR SOMEONE WHO MAKES YOU SMILE.  Because it takes only a smile to make duck days bright. Hope you will find someone who will makes you smiles. 

Monday, April 15, 2013

Kuna tabia hatari mno kwenye uhusiano wa kimapenzi, zisome uzijue

Tunazungumzia mapenzi katika sura ya kipekee kwa kuwa yanahitaji thamani ya hali ya juu. Yanaheshimiwa kupita kiasi kwa sababu yenyewe ni sanaa kiranja ambayo kila mtu lazima atayapitia.

Tunapenda na kupendwa, hivyo tupo mapenzini. Ambaye hayumo, basi pengine mambo yake siyo mazuri. Hata hivyo, binadamu hatuko sawa, kila mtu anayo tafsiri yake anayoijua kuhusiana na mapenzi, ndiyo maana hatuachi kuelekezana. Naandika kwa kushauri na kukosoa kwa sababu huu ndiyo wajibu wangu katika safu hii.

Kila mmoja anapoingia katika uhusiano wa kimapenzi, moja kwa moja ndoto zake huwa ni kumfanya mwenzi wake kuwa wa kudumu. Atajiwekea malengo hata yasiyotekelezeka ilimradi airidhishe nafsi yake.

Hujawahi kuona mtu anapata mwenzi leo, kisha akaanza kupiga mahesabu ya kufunga naye ndoa? Ukweli ni kwamba wengi wetu tunapopata penzi jipya, tunakuwa na matarajio mengi. Ni vizuri kuwa na matarajio na kujiwekea malengo ya kuyatimiza, lakini kosa kubwa ni kwamba huwa tunajisahau katikati ya safari.

Tunapenda kudumu na wenzi wetu tunaowapata, lakini ndoto hizo hugeuka za alinacha kama si kitendawili kwa kuwa hatuwezi kujirekebisha au kuficha makucha. Matunda ya hali hiyo ni kuwa na kizazi chenye kujiwekea matarajio ya ‘blah blah’ kila siku.

Pointi ya msingi hapa kama kweli tunataka kuwa na mapenzi ya kudumu ni kujua udhaifu wetu angali bado mapema. Kutambua mambo ambayo ni sumu, zinayoweza kuuua uhusiano wetu ili tuzichukue kama changamoto, kisha tuzikabili na kushinda.

Hapa chini, nimekuandalia tabia 10 ambazo ni sumu katika mapenzi. Hizi, zinaweza kuubomoa uhusiano wako ndani ya muda mfupi. Muhimu ni kuzijua ili utambue namna ya kuziepuka.

Unaweza kuziepuka kwa sababu siyoo maumbile, bali ni kujiendekeza. Ukiamini hakuna kitakachoshindikana, kwahiyo nakuasa uongozane na mimi mdogo mdogo ili upate jawabu la kutosha kuhusiana na mada hii.

UVIVU

Hii ni sumu kali, lakini ni rahisi kuiepuka kama utaamua. Asili ya umbile la kila binadamu, ndani yake kuna uvivu. Na ni vizuri kutambua kuwa katika vitu ambavyo ni rahisi kumchefua mwenzi wako ni hili la uvivu.

Uvivu unaweza kuwa wa kujishughulisha katika mambo ya nyumbani ama wa utafutaji wa riziki. Lakini baki ukijua kwamba tabia hiyo inakufanya ukalie kuti kavu kwenye uhusiano wako

Unashindwa kumsaidia mpenzi wako kazi ndogo ndogo, unangaalia nguo chafu haujitumi kuzifua, nyumba haitamaniki, hujiwezi kwa lolote, tabia yako hiyo, inampa mwenzio tiketi ya kukuacha.

Pointi hii, inastahili kupigiwa mstari mwekundu kwetu sisi wanawake. Ni rahisi mwanaume kuvumilia kasoro chache alizonazo mwenzake, lakini siyo ya namna hii. Muhimu ni kutambua ya kwamba uvivu utakupunguzia heshima na mvuto wako katika mapenzi.

Aidha, kwa mwanamke ni janga ambalo mwanaume hatokawia kulikimbia. Unadhani atawezaje kuvumilia kuwa na mtu ambaye hajiwezi kwa lolote? Kujishughulisha hutaki, kuwajibika katika uwanja wa kuta nne ni ngoma nzito! Atajiuliza: Ni faida gani ya kuwa na wewe?

UCHAFU

Tabia hii, inaenda sambamba na uvivu. Kwa kifupi ni kwamba uchafu ni matokeo ya uvivu. Mtu asiyejiweza kwa lolote hatomudu usafi, hivyo kutia sumu kwenye uhusiano wake.

Una tabia ya uvivu, kwahiyo ni mchafu, unapaswa kutambua kuwa mwenzi wako anakerwa mno na tabia yako. Anza kwa kujichunguza mwenyewe ili kujua wewe ni mchafu kwa kiwango gani. Jawabu lako, linaweza kukusaidia kwa kiasi cha kutosha, ikiwa utaamua kubadilika.

Unavaa nguo mpaka zinatoa harufu mbaya, ukiongea, unatoa hewa chafu ya mdomo, kuoga kwa wasiwasi hadi mwili unanata, unashindwa kudhibiti jasho lako, mpaka unawasumbua wenzako kwa sababu ya kikwapa, kwa hali hiyo unategemea nini?

Tuweke kituo kikubwa kwa leo, panapo majaliwa tukutane Jumatatu, tupate kuendelea na mada yetu hii. Ushirikiano wako bado nauhitaji, kwahiyo tumia namba yangu hapo juu kwa ushauri au maoni.

Kama utakumbuka vizuri shoga yangu, katika toleo lililopita la Ijumaa Wikienda, niliweza kuchambua sumu mbili kati ya 10 zinazounda mada hii. Sina shaka kwamba ulinisoma vya kutosha, hivyo nakuomba uungane nami tena leo ili tuendelee pale tulipoish

Nilieleza Uvivu na Uchafu kama sumu zinazoshabihiana, kwahiyo zimebaki nane. Kabla sijaendelea mbele, naona ni busara nikuulize swali moja; Umejifunza nini mpaka sasa, kutokana na mada hii? Jibu naomba unitumie kupitia namba ya simu iliyopo hapo juu.

UBISHI

Unyenyekevu ni mbolea ya mapenzi, kinyume chake ni sumu, ndiyo maana ubishi ukawa tindikali ya uhusiano. Changamoto hii, kama ingekuwa inaeleweka vizuri na kuzingatiwa inavyotakiwa, pengine kusingekuwa na watu wanaotengana.

Binadamu tumeumbwa na udhaifu, kwahiyo kukosea siyo vibaya kwakuwa ni sehemu ya maisha yetu. Pamoja na kulifahamu hilo, lakini wengi wetu huwa hatutaki kukubali ukweli katika yale tunayokuwa tumekosea.

Tunataka tushinde kwa hoja hata kwenye mambo ambayo tunastahili kuwaomba radhi wapenzi wetu. Kasumba ya namna hiyo huwaumiza wenzetu moyoni kwa sababu wao huamini wamekosewa, kwahiyo hutarajia angalau kuombwa msamaha.

Fikiria mpenzi wako amekufanyia kosa ambalo wewe unalitathmini kama ni kubwa, unamuweka chini unaongea naye, lakini mwenzako anakuruka futi hamsini. Hataki kukubali kosa na zaidi anataka mbishane mpaka majogoo yawike. Katika picha ya namna hiyo wewe utajisikiaje?

Maumivu utakayoyapata wewe, basi yaone kuwa ndiyo anayopata mwenzako kutokana na tabia yako ya kutotaka kukubali ukweli. Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, msemo huu una maana kubwa kwa sababu tunapenda kuwaona wengine wabishi, lakini yakiwa kwetu hatutaki kujikosoa.

KIBURI

Kama ilivyo uchafu unatokana na uvivu, ndivyo ilivyo kwa Ubishi unavyoleta Kiburi. Maana yake ni kwamba mtu unapokuwa mbishi kupitiliza, unavimba kichwa na huko ndiko kuelekea kwenye kiburi. Utaelezwa nini na wewe kila kitu unajua?

Asili ya mtu mwenye kiburi huwa na majivuno kwa kuamini kwamba hakuna kinachoweza kumbabaisha. Lakini mtu mwenye fikra hizi anakuwa amepigwa kikumbo na tafsiri ya mapenzi ambayo inasema ni mwiko kujifanya ‘much know’ mbele ya mwenzi wako.

Daima kila unaloelekezwa hufanyi, badala yake unakuwa mzuri katika kupuuzia mambo. Ukichekecha kichwa chako, utagundua kwamba upuuzi ni sehemu ya kiburi, mnapanga miadi wewe na sweetie wako mkutane mahali, lakini mwisho wa siku unaamua kutokwenda bila sababu ya msingi.

Mpo katika maongezi ya faragha, mwenzio anajaribu kukuelewesha katika maeneo ambayo huwa unakosea, lakini badala ya kupokea ukweli, unaamua kunyamaza kimya, halafu unamkunjia sura kana kwamba anachokwambia ni simulizi za kubuni. Hicho ni kiburi!

Ukweli upo hivi, mtu mwenye kiburi akiambiwa ukweli huamini ametukanwa, hivyo huzua visa vya uongo na ukweli ama kubisha bila hoja, ndiyo maana nilitangulia kusema kuwa kiburi ni zao la ubishi.

Kasumba hii ukiwa nayo ni rahisi kuachwa kwa sababu hakuna siku ambayo mpenzi wako atakuwa anajisikia faraja kuwa na wewe. Atakuona mzigo kwakuwa ataamini haumheshimu na ukichunguza inakuwa kweli, kwani ungekuwa unamtii, usingembishia ama kumvimbia kwa kiburi chako.

NYODO

Najaribu kuzipanga pointi katika mtiririko unaofaa, nikiamini kuwa ndiyo itakuwia rahisi kuelewa. Aghalabu, mtu mwenye kiburi ndiye huyo huyo mwenye nyodo. Unakuwa bingwa wa mapozi na michetuo mbele ya mwenzi wako, lakini mapenzi hayataki hivyo!

Hakuna kitu kibaya kama kujiona babkubwa katika mapenzi, saikolojia inafundisha kwamba ukiwa memba katika uhusiano fulani, basi unatakiwa kuishi kulingana na jinsi ulivyo. Tafsiri ya sentensi hiyo ni kuwa unashauriwa kuishi rahisi, kutokana na jinsi alivyo mpenzi wako.

Si busara ukiwa na mwenzi wako, halafu unakuwa unaongelea mambo makubwa ambayo haoti kuyaona sembuse kuyapata. Au unakuwa bingwa wa kubagua chakula, kwa kukiona ni cha gharama nafuu, huku ukiwa kiongozi wa kuomba misosi ya bei mbaya.

Mpenzi wako anajitutumua anakununulia zawadi, badala ya kushukuru, mwenzetu unapokea huku ukibetua midomo kuonesha kwamba siyo za hadhi yako. Picha hiyo, ukimuonesha mara tatu, halafu akiendelea kukupa zawadi, pengine huyo mwenzako atakuwa na matatizo kichwani.

Anapanga vizuri mambo yake, anakuomba mtoke wote, mnafika kiwanja, unaanza kukishusha thamani, halafu unakosa raha kabisa kuwepo eneo husika. Taswira kama hiyo unapomuonesha mwenzako, itamvunja moyo na atajuta kutoka na wewe.

Muhimu hapa ni kuridhika na kile unachopewa, hivyo ndivyo mapenzi yanataka. Anachokupa shukuru kwakuwa ndicho alichojaliwa, siku akipata zaidi atakupa cha thamani kubwa. Kinyume chake ni kumkera kwakuwa atakuona una nyodo na haufai kuwa mpenzi wa kudumu.

DHARAU

Hapo juu nimeshaeleza kuwa NYODO inatokana na KIBURI kwa sababu mtu mwenye nyodo na kiburi ni kama shati na fulana au viatu na soksi.

Sura hiyo, ndiyo iliyopo katika DHARAU na NYODO. Ni kama shamba na bustani, nikiwa namaanisha kwamba tabia hizi zinatafsiri zenye kukaribiana, lakini nazitofautisha katika mada hii ili kila moja ibebe uzito wake.

Dharau ni sumu kubwa katika uhusiano wowote. Ukiwa na sifa hii, unatakiwa kujishtukia kuwa wewe ni vigumu kukubalika mbele ya mtu mwingine yeyote na zaidi ni katika mapenzi, kwani hakuna atakayeweza kukuvumilia.

Kikubwa hapa ni kujua kuwa mara unapokuwa katika uhusiano na mtu fulani, basi yule ni mwenzako. Shirikiana naye katika hali zote. Kama ana upungufu, jukumu lako ni kuubaini mapema na kujitahidi kuurekebisha. Kumzodoa ni alama ya dharau.

Marekebisho, yawe ni katika kila unaloona halikupendezi kutoka kwake, yawezekana mavazi yake yakawa yanakupa kichefu chefu, kwahiyo unapaswa kulivalia njuga suala hilo ili umuweke mpenzi wako kwenye sura ambayo inakuvutia.

Kumshusha thamani ni dharau na ukimuonesha akaelewa unamdharau, hiyo ni sumu kali katika uhusiano wako. Ni vizuri kutambua kwamba mapenzi ni sanaa inayojengwa kwa hisia, kwahiyo kudumu ama kutokudumu kwa penzi lako, kutategemea na wewe na unavyocheza na hisia za mwenzako.

Hupendi staili yake ya maisha, hilo ni jukumu lako. Maisha ya nyumbani kwao ni ya shida, elewa hali hiyo ni matokeo na kwamba kupata ni majaliwa. Anaumwa yeye mweyewe, mzazi ama ndugu yake yeyote, ni vizuri kutambua kuwa kabla hujafa hujaumbika.

Ukijua hayo, basi hutomtoa kasoro mwenzako na badala yake utashiriki kumsadia pale unapoweza. Ukifanya kinyume chake ni ishara nyingine ya dharau na akijua unamuona wa bei chee ataona unamyanyapaa.

UONGO

Tafsiri yake ni tabia ya kutosema ukweli, yaani ujanja mwingi na kudanganya ili kujiweka katika mazingira salama. Pamoja na ukweli kwamba wengi huutumia katika kujipa ushindi wa mezani, lakini hii ni sumu nyingine kali kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Maana nzuri katika tafsiri fupi ni kuwa uongo ni dharau kwakuwa angemheshimu, asingemdanganya. Mtu anayemuongopea mpenzi wake, huyo si muoga kwenye uhusiano, hivyo anakuwa amepitwa na nguzo muhimu ya kulifanya penzi lake lidumu kwa miaka mingi.

Ukichunguza kwa makini, asilimia kubwa ya watu waliodumu na wenzi wao ni wale wanaoishi kwa hofu katika uhusiano. Anauheshimu, kwahiyo anaogopa kuuvunja. Anaweka mikakati ya kujiweka salama mbele ya laazizi wake. Lakini hayo si ndiyo mapenzi?

Aidha, ukichunguza tena kwa makini, utabaini kuwa uongo, maana yake ni kujiona unajua vitu vingi kuliko wengine. Wewe ni fundi wa kugeuza maneno na unaweza kumfanya mtu aamini moja jumlisha moja ni tatu. Lakini mapenzi hayataki hivyo!

Wengi huuchukulia uongo kama chachandu ya mapenzi, huku asilimia kubwa wakiufanya kuwa sehemu ya maisha yao. Je, hujawahi kumuona mtu asiyejua kusema ukweli? Na kila akibadilisha pointi, anapandisha uongo juu ya uongo?

Jibu; watu wa aina hiyo ni wengi, wamejaa kila sehemu, lakini ni busara kujiuliza swali lingine, unadhani wanapata faida? Jawabu lake ni kuwa inawezekana kupata faida, lakini mbona wengi wao waliishia kuumbuka? Akili kumkichwa!

Unatoka nje, ukirudi unadanganya, unasema uongo ili kumnasa ndege wako, lakini lazima ukumbuke kuwa za mwizi ni arobaini.

UJUAJI

Ufundi kujua ni hatari kwa sababu mwenye tabia hii, hutaka aonekane yeye ndiye anayejua kila kitu. Hii ni kinyume na tafsiri ya mapenzi ambayo inaelekeza usawa kwa wawili wapendanao na kila mmoja aamini na kuthamini fikra na hisia za mwenzake.

Kila mada inayotua mezani wewe ndiye msemaji mkuu, hili lazima litamkera mwenzako. Mbaya zaidi, unajitia ujuaji katika mambo ambayo hupaswi kujiweka kimbelembele. Kauli zako, zinaweza kumpa picha kuwa wewe siyo chaguo lake sahihi.

Ujuaji ni pointi inayorandana na ubishi, kwa sababu tafsiri ya mtu anayebisha sana ni kuwa yeye ni mjuaji wa kila kitu. Lakini unadhani sifa hii itamfikisha popote? La hasha!

Ni mmoja kati ya 10, anayeweza kumudu vishindo vya mtu anayejifanya ‘much now’.

Kisaikolojia, kila mtu ana asili ya kujiona bora kuliko mwingine, hata kama hajioneshi, lakini lazima zitakuwepo chembechembe ndani yake, zinazompa kiburi kwamba yeye ndiye namba moja. Lakini wapo waliopitiliza.

Huyu aliyepitiliza, akikutana na aliyepitiliza mwenzake, lazima moto utawaka. Kadhalika hata akipambana na yule mwenye ujuaji wa siri, picha lazima iende segemnege kwa sababu hakuna atakayekubali kuburuzwa.

STAREHE

Penzi lako linaweza kudumu kutokana na aina ya mtu uliyenaye. Si wote wanaochukia starehe, kwani wengine kujirusha ndiyo sehemu ya maisha yao. Kama mpenzi wako anapenda kubadili viwanja na wewe ukawa hivyo, basi upele utakuwa umepata mkunaji.

Aghalabu, ni bora mwanaume awe anapenda starehe halafu kwa mwanamke ikawa ni kinyume chake, hii inatokana na asili ya maumbile ya jinsia hizi mbili kuwa ni rahisi mke kumvumilia mume mpenda anasa, anayejirusha usiku kucha.

Mwanaume hawezi kumvumilia mpenzi wake anayebadili viwanja usiku wa manane, kwani akimsamehe mara moja, basi inayofuata atamrudishia mlangoni. Katika hali kama hiyo, unadhani mapenzi yanaweza kuendelea kuwepo?

Ifahamike kuwa si mwanaume pekee mwenye kuthubutu kumtimua mpenzi wake ambaye anapenda starehe, bali, wapo pia wanawake wenye ghadhabu na maisha, kwahiyo kuwa na wanaume wanaoteketeza hela katika mambo ya anasa huona kama wanachezea maisha. Unadhani uamuzi wao ni upi? Jibu; Kuanza mbele!

USALITI

Ni mara chache mtu afumaniwe kisha aendelee kuwepo kwenye uhusiano wake. Katika hali ya kawaida, mtu anapobainika amesaliti, basi hiyo ndiyo talaka yake. Sasa je, katika ukweli wa hali ya sasa, ni wangapi waaminifu?

Jibu; Labda mmoja kati ya watano na pengine tathmini ikawa juu ya hapo. Lakini hiyo siyo pointi ya kukufanya ujione upo sahihi kwa sababu watenda dhambi ni wengi, badala yake jiulize hivi: “Kwanini niishi kwa kumuumiza mpenzi wangu?”

Za mwizi arobaini, siku ukikamatwa utapigwa chini, hata kama atakusamehe, lakini utaishi ukijua kwamba umeshatia doa katika uhusiano wako. Pia, unapaswa kujua kuwa usaliti wako, unaweza kumpa hamasa na yeye aanze kucheza ‘gemu’ la nje. Hali ikashakuwa hivyo, je, hapo kuna mapenzi?

Ni vizuri kuishi kwa uaminifu, kwani maisha ya mapenzi ndivyo yanavyotaka.

Sunday, September 30, 2012

WANAUME HUPENDA KUOA MWANAMKE WA AINA HII




 

WANAUME HUPENDA KUOA MWANAMKE WA AINA HII
Habari za wiki hii mpenzi msomaji. Mimi namshukuru Mungu kwa kuweza kunikutanisha na nyinyi kupitia safu hii ambayo pamoja na mambo mengine nazungumzia juu ya mada mbalimbali ambazo zinagusa maisha yetu ya kila siku.
Wiki hii nitazungumazia juu ya aina ya wanawake ambao wanaume wengi hupendelea kuoa. Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa. Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.

 
MWEYE MAPENZI YA KWELI
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara ndio wamekuwa furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake. Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingi utamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.
Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha  siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.
 
Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya  maisha ya  ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia  ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha ya raha mustarehe.
 
WENYE TABIA NZURI
Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja suala na kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini  wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa  anatabia mbaya. Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya  wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.
Si hivyo tu wapo wanaume  ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.
 
WENYE UCHU NA MAENDELEO
 
Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani 'golikipa'. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini. Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.
 
WASIOPENDA MAKUU
 
Kuna  wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia "leo tunakwenda wapi dear?"  Akimuona rafiki yake kanunua simu ya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama  ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia, "mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho  nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.

 
Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa  kuwaoa.  Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu fulani.’
Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa  tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi  ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.
Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leo amemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.
Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitaji upo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulani wakati inawezekana uwezekano haupo.
 
WAVUMILIVU
Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotea kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?
 
Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.
 
Licha ya kupenda kuoa wanawake amabo wana tabia hizo nilizozitaja hapo juu, wanachukizwa sana na wanawake ambao wanavijitabia vidogo vidogo ambavyo kimsingi havikubaliki katka jamii.Tabia hizo ni kama wambea, wasio wakweli na wawazi, wasioridhika, wagumu kusamehe na wapesi wa kuchukia, wagomvi na wenye roho ya kwanini.
 Utafiti huu umefanyikwa kwa baadhi ya wanaume ambao wanatarajia kuoa wanawake ambao wanaoishi katika maeneo mbalimbali jijini Dar-es-Salaam. Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.

Tuesday, July 24, 2012

What is RuralCyberSpace by the way?

Rural Cyber Space is new young aged emerging company which is coming at all force to take the control of the Information Technology Market. The aim of this company is to provide Information Technology product which satisfy the needs of the market.
The world is has already undergone technology revolution, at the third party countries it seems like we are ten years back, we need  more effort in order to cover the distance in which we are back in terms of technology
Take a look at developed countries and see your self how far are we. Teachers are no longer  marking student exams manually, what has left in their hands is just to teach, all remaining activities are computerized.
To say technology revolution has simplified how every thing is conducted is not enough, but is also more pleasure to say technology revolution is more than every you are thinking right now.

Wellcome To The World Of IT